Part 2
142. WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza
kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na
Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo
nyooka.
143. Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa
wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu
yenu. Na hatukukifanya kibla ulicho kuwa nacho ila
tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka akarejea nyuma. Na kwa yakini
144. Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso
wako mbinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho.
Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na
popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; na hakika wale walio pewa
Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi
Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo
yatenda.
145. Na hao walio pewa Kitabu, hata ukiwaletea hoja za kila namna,
hawatafuata Kibla chako; wala wewe hutafuata kibla chao, wala baadhi yao
hawatafuata kibla cha wengineo; na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya
kukufikia ujuzi, hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhullumu.
146. Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya
147. Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka.
148. Na kila mmoja anao upande anao elekea. Basi
shindanieni mema. Popote mlipo Mwenyezi Mungu
atakuleteni nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Muweza wa kila kitu.
149. Na popote wendako elekeza uso wako
kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa
Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na
mnayo yatenda.
150. Na popote wendako elekeza uso wako
kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio
dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate
kuongoka.
151. Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana na
nyinyi, anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na
hikima na kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui.
152. Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na
nishukuruni wala msinikufuru.
153. Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa
subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na
wanao subiri.
154. Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu
ni maiti; bali hao ni wahai, lakini
nyinyi hamtambui.
155. Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa
156. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.
157. Hao juu
158. Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni
katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anaye hiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya
Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anaye jitendea mwenyewe kheri basi bila ya
shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mjuzi.
159. Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha -- nazo ni hoja zilizo
wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani
Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye
kulaani.
160. Ila wale walio tubu na wakatengeneza na
wakabainisha, basi hao nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea
toba na Mwenye kurehemu.
161. Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu
162. Watadumu humo. Hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa kupumzika.
163. Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana
mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye
kurehemu.
164. Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana
usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na
maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha
ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika
mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi,
bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.
165. Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi
Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu.
Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi
166. Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano
167. Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa
wao
168. Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.
169. Yeye anakuamrisheni maovu na machafu, na
mumsingizie Mwenyezi Mungu mambo msiyo yajua.
170. Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao
husema:
171. Na mfano wa walio kufuru ni kama mfano wa
anaye mpigia kelele asiye sikia ila wito na sauti tu -- ni viziwi,
mabubu, vipofu, kwa hivyo hawaelewi.
172. Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye
tu.
173. Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na
kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana
dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe,
Mwenye kurehemu.
174. Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika
Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa
moto, wala Mwenyezi Mungu hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao watapata adhabu chungu.
175. Hao ndio walio nunua upotofu badala ya uwongofu, na adhabu badala ya maghfira. Ama wavumilivu wa Moto watu hawa!
176. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu
ameteremsha Kitabu kwa haki. Na wale walio khitilafiana katika Kitabu wamo
katika upinzani ulio mbali na haki.
177. Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa
mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya
Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake,
jamaa na mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na
akawa anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na
wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio
sadikisha, na hao ndio wajilindao.
178. Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa
- muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na
mwanamke kwa mwanamke. Na anaye samehewa na ndugu yake
chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kuliko tokana na Mola wenu Mlezi, na ni
rehema. Na atakaye vuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu
chungu.
179. Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.
180. Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na
mauti, kama akiacha
181. Na atakaye ubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakao ubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kusikia Mwenye kujua.
182. Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi
akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye
kurehemu.
183. 183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu,
184. (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na
atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika
siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa
kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa
kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora
kwenu,
185. Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni
uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na
upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge.
Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine.
Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa
amekuongoeni ili mpate kushukuru.
186. Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi
nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba.
Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate
kuongoka.
187. Mmehalalishiwa usiku wa Saumu
kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi
ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini
nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na
amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni
aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na
kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni
mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu
anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate
kumcha.
188. Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu
ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na
hali mnajua.
189. Wanakuuliza khabarai ya miezi. Sema: Hiyo ni
vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hija. Wala sio wema kuziingia nyumba kwa nyuma.
190. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na
wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu
hawapendi waanzao uadui.
191. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe
popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko.
Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
192. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
193. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na
Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na
194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni
nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu
pamoja na wachamngu.
195. Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na
fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao
wema.
196. Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu. Na ikiwa mkizuiwa,basi (chinjeni)
wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu
mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakaye kuwa mgonjwa au ana
vya kumuudhi kichwani mwake basi atoe fidiya kwa
kufunga au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama. Na mtakapo kuwa salama, basi
mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio
akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiye pata, afunge siku
tatu katika Hija na siku saba mtakapo rudi; hizi ni
kumi kaamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu
wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
197. Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia
kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye
vitendo vichafu wala asibishane katika Hija. Na kheri yoyote
mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na jitengezeeni
zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu.
Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!
198. Si vibaya kwenu kuitafuta fadhila ya Mola wenu Mlezi. Na mtakapo miminika kutoka A'rafat mtajeni Mwenyezi Mungu penye
Masha'ril Haram. Na mkumbukeni kama alivyo
kuongoeni, ijapo kuwa zamani mlikuwa miongoni mwa walio potea.
199. Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminika watu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha: hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
200. Na mkisha timiza ibada zenu basi mtajeni Mwenyezi Mungu
201. Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani
mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya
Moto!
202. Hao ndio watakao pata sehemu
203. Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa.
Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye
kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba
nyinyi mtakusanywa kwake.
204. Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa
maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa
yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu.
205. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa
kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi
Mungu hapendi ufisadi.
206. Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo
inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa
mapumziko.
207. Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa
kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
208. Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa
ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye
wazi.
209. Na ikiwa mkateleza baada ya kukufikieni hoja zilizo wazi, basi
jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye
hikima.
210. Je wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya
mawingu pamoja na Malaika, na hukumu iwe imekwisha
tolewa? Na kwa Mwenyezi Mungu ndio hurejeshwa mashauri
yote.
211. Waulize Wana wa Israili: Tumewapa
ishara ngapi zilizo wazi? Na anaye zibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya
kumfikia basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa
kuadhibu.
212. Walio kufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na
wanawafanyia maskhara walio amini. Na wenye kuchamngu watakuwa juu
213. Watu wote walikuwa ni umma mmoja.
Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii wabashiri na
waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili
kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala
hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho
baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina
214. Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni
215. Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na
wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu
anaijua.
216. Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda
mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda
mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu
anajua na nyinyi hamjui.
217. Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema:
Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini
kuzuilia watu wasende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na
kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye Msikiti Mtakatifu na
kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala hawatoacha kupigana nanyi
mpaka wakutoeni katika Dini yenu
218. Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia
ya Mwenyezi Mungu, hao
ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
219. Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari.
Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa
watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa
yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho
chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate
kufikiri--
220. --katika mambo ya dunia na mambo ya
Akhera. Na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema:
Kuwatengenezea ndio kheri. Na mkichanganyika nao basi ni
ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angeli penda angeli kutieni katika udhia.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye
hikima.
221. Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi
Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni.
Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini.
Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina
hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na
Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye
huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka.
222. Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni
uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha
t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao
jisafisha.
223. Wake zenu ni
224. Wala msifanye jina la Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa ni kisingizio cha kuacha kufanya wema na kuchamngu na
kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kusikia na Mwenye kujua.
225. Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu
vya upuuzi.
226. Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake
zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
227. Na wakiazimia kuwapa talaka basi, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mjuzi.
228. Na wanawake walio achwa wangoje peke
229. T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri. Wala si halali
kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila
ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya
Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na
mipaka ya Mwenyezi Mungu hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa.
Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na
watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhaalimu.
230. Na
231. Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala
msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye
fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu,
na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anacho
kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni
kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
232. Na mtakapo wapa wanawake t'alaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina
233. Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili
kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba
yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa
ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo
wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala
baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa
hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa
kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia
watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya
kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo
yatenda.
234. Na wale miongoni mwenu wanao kufa na
wakaacha wake, hawa wake wangoje peke
235. Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa
ishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini
msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu.
Basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.
236. Hapana ubaya kwenu mkiwapa t'alaka wanawake ambao hamjawagusa au
kuwabainishia mahari
237. Na mkiwapa t'alaka kabla ya kuwagusa, na
mmekwisha wawekea hayo mahari makhsusi, basi wapeni nusu ya mahari mlio agana,
isipo kuwa ikiwa wanawake wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa
ki mikononi mwake awe amesamehe. Na kusameheana ndiko kulio karibu zaidi na uchamngu. Wala msisahau fadhila baina
yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
238. Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na
simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti
(kunyenyekea).
239. Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali
mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni
Mwenyezi Mungu
240. Na wale miongoni mwenu wanao kufa na
wakawacha wake, na wausie kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja
bila ya kuwatoa nyumba. Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu
kwa waliyo jifanyia wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
241. Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa
mujibu wa Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu.
242. Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.
243. Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa
maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha
akwahauisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye
fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
244. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na
jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Msikizi na Mjuzi.
245. Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na
hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea.
246. Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipo
mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika
Njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: Je, haielekei ikiwa mtaandikiwa vita kuwa
msipigane? Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali tumetolewa majumbani kwetu na watoto wetu? Lakini
walipo andikiwa kupigana waligeuka, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu.
247., Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Mungu amekuteulieni Taluti
(Sauli) kuwa ni mfalme. Wakasema: vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi
tuna haki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa
248. Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni
kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho
kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina
Harun, wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo
dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini.
249. Basi Taluti alipo ondoka na majeshi
alisema: Mwenyezi Mungu atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja
nami, na asiye kunywa atakuwa pamoja nami: ila atakaye
teka kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo
isipo kuwa wachache tu miongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na wale walio amini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi
Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi mangapi madogo yameshinda makundi
makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
250., Na walipo toka kupambana na Jaluti na
majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na
isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri--
251. --Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na
Daudi akamuuwa Jaluti, na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hikima, na
akamfundisha aliyo yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeli haribika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote.
252. Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu
tunakusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa
Mitume.