105 - AL - FIIL
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye
tembo?
2. Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?
3. Na akawapelekea ndege makundi kwa
makundi,
4. Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
5. Akawafanya kama majani yaliyo
liwa!