109 - AL - KAFIRUN
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Sema: Enyi makafiri!
2. Siabudu mnacho kiabudu;
3. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
4. Wala sitaabudu mnacho abudu.
5. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini
yangu.