113 - AL - FALAQ
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa
mapambazuko,
2. Na shari ya alivyo viumba,
3. Na shari ya giza la usiku liingiapo,
4. Na shari ya wanao pulizia
mafundoni,
5. Na shari ya hasidi anapo husudu.