12 - YUSUF
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
2. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate
kuzingatia.
3. Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na
ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua.
4. Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota
nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.
5. (Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako,
wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa
mwanaadamu.
6. Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha
tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub,
7. Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanao
uliza.
8. Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na
baba yetu kuliko sisi, hali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo
katika upotofu wa dhaahiri.
9. Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu
ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwa watu wema.
10. Akasema msemaji kati
11. Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na
hakika sisi ni wenye kumtakia kheri!
12. Mpeleke kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze; na bila ya
shaka sisi tutamhifadhi.
13. Akasem: Kwa hakika inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na
ninaogopa asije mbwa mwitu akamla nanyi mmeghafilika naye.
14. Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kundi lenye
nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa khasarani.
15. Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya
kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao
hili, na wala wao hawatambui.
16. Wakaja kwa baba
17. Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na
tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe
hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli.
18. Wakaja na kanzu yake ina damu ya uwongo. Akasema:
19. Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza
ndoo yake. Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya
ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayo yatenda.
20. Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa akali ya pesa. Wala hawakuwa
na haja naye.
21. Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee
makaazi ya hishima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu. Na
22. Na alipo fikilia utu uzima tulimpa hukumu na ilimu. Na
23. Na yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha
nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi!
Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika
wenye kudhulumu hawatengenekewi.
24. Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau
kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na
uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa.
25. Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akairarua
kanzu yake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema:
Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au
kupewa adhabu chungu.
26. Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na
shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa
mbele basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.
27. Na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema
uwongo, naye Yusuf ni katika wakweli.
28. Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma,
alisema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi
vyenu ni vikuu.
29. Yusuf! Wachilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa
dhambi zako. Kwa hakika wewe ni katika walio fanya makosa.
30. Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa
anamtamani mtumishi wake ! Hakika amesalitika kwa mapenzi. Sisi hakika
tunamwona yumo katika upotovu ulio dhaahiri.
31. Alipo sikia yule bibi masengenyo yao aliwaita, na akawawekea
matakia ya kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza
mbele yao. Basi walipo mwona waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikata
mikono yao. Wakasema: Hasha Lillahi! Huyu si mwanaadamu. Hakuwa huyu ila ni
Malaika mtukufu.
32. Yule bibi aksema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli
mimi nilimtaka naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka
atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa.
33. Yusuf akasema: Ee Mola Mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko
haya anayo niitia. Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao,
na nitakuwa katika wajinga.
34. Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao.
Hakika Yeye ni Msikizi Mjuzi.
35. Basi ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara kuwa wamfunge kwa
muda.
36. Wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema:
Hakika mimi nimeota nakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Mimi nimeota nimebeba
mikate juu ya kichwa changu, na ndege wanaila. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani
sisi tunakuona wewe ni katika watu wema.
37. Akasema: Hakitakufikilieni chakula mtakacho pewa ila
nitakwambieni hakika yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale aliyo
nifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasio muamini
Mwenyezi Mungu, na wakawa hawaiamini Akhera.
38. Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub.
Hatuna haki ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila
ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu; lakini watu wengi hawashukuru.
39. Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi wanao farikiana
wao kwa wao ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu?
40. Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba
zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila
ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu.
Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.
41. Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana
wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake.
Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza.
42. Na akamwambia yule aliye jua kuwa atavuka katika wale wawili:
Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shet'ani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana
wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa.
43. Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba
wanene wanaliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine
makavu. Enyi waheshimiwa! Nambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza
kuagua ndoto.
44. Wakasema: Hizi ni ndoto zilizo paraganyika, wala sisi sio wenye
kujua tafsiri ya ndoto hizi.
45. Hapo akasema yule aliye okoka katika wale wawili akakumbuka
baada ya muda: Mimi nitakwambieni tafsiri yake. Basi nitumeni.
46. Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze nini maana ya ng'ombe saba wanene
kuliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu,
ili nirejee kwa watu wapate kujua.
47. Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni
katika mashuke yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula.
48. Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayo kula kile
mlicho iwekea isipo kuwa kidogo mtacho kihifadhi.
49. Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu
watasaidiwa, na watakamua.
50. Na mfalme akasema: Mleteni kwangu! Basi mjumbe alipo mjia Yusuf
alisema: Rejea kwa bwana wako ukamuulize khabari ya wale wanawake walio jikata
mikono yao. Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao.
51. Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipo mtaka Yusuf kinyume na
nafsi yake? Wakasema: Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa
Mheshimiwa akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliye mtaka kinyume na
nafsi yake, na hakika yeye ni katika wakweli.
52. Hayo ni apate kujua ya kwamba mimi sikumfanyia khiyana nyuma
yake; na ya kwamba Mwenyezi Mungu haziongoi hila za makhaini.
53. NAMI sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu,
isipo kuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi
ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.
54. Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa.
Basi alipo msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na
umeaminika.
55. Yusuf akasema: Nifanye mshika khazina za nchi. Kwani hakika mimi
ni mlinzi mjuzi.
56. Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo
popote anapo penda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo
ya wafanyao mema.
57. Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa walio amini na
wakawa wachamngu.
58. Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na
wao hawakumjua.
59. Na alipo watengenezea tayari haja yao alisema: Nileteeni ndugu
yenu kwa baba. Je! Hamwoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa
kukirimu?
60. Na msipo niletea basi hampati kipimo chochote kwangu, wala
msinikurubie.
61. Wakasema: Sisi tutamrairai baba yake; na bila ya shaka tutafanya
hayo.
62. Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika
mizigo yao, ili wazione watakapo rudi kwa watu wao wapate kurejea tena.
63. Basi walipo rejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu!
Tumenyimwa chakula zaidi, basi mpeleke nasi ndugu yetu ili tupate kupimiwa; na
yakini sisi tutamlinda.
64. Je, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye
zamani? Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa
kurehemu kuliko wenye kurehemu wote.
65. Na walipo fungua mizigo yao wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa.
Wakasema: Ewe baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa.
Wacha tuwaletee watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza
shehena ya ngamia. Na hicho ni kipimo kidogo.
66. Akasema: Sitampeleka nanyi mpaka mnipe ahadi kwa Mwenyezi Mungu
kwamba lazima mtamrejeza kwangu, ila ikiwa mmezungukwa. Basi walipo mpa ahadi
yao alisema: Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.
67. Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni
kwa milango mbali mbali. Wala mimi sikufaeni kitu mbele ya Mwenyezi Mungu.
Hukumu haiko ila kwa Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu
yake Yeye wategemee wanao tegemea.
68. Na walipo ingia kama alivyo waamrisha baba yao, haikuwafaa kitu
kwa Mwenyezi Mungu, isipo kuwa ni haja tu iliyo kuwa katika nafsi ya Yaa'qub
aliitimiza. Na hakika yeye alikuwa na ilimu kwa sababu tulimfundisha; lakini
watu wengi hawajui.
69. Na walipo ingia kwa Yusuf alimchukua nduguye akasema: Mimi
hakika ni nduguyo. Basi usihuzunike kwa waliyo kuwa wakiyafanya .
70. Na alipo kwisha watengenezea mahitaji yao akakitia kikopo cha
kunywea maji katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mnadi akanadi: Enyi wasafiri!
Hapana shaka nyinyi ni wezi!
71. Wakasema nao wamewakabili: Kwani mmepoteza nini?
72. Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na ataye lileta atapewa
shehena nzima ya ngamia. Nami ni dhaamini wa hayo.
73. Wakasema: Wallahi! Mnajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya
uharibifu katika nchi hii, wala sisi si wezi.
74. Wakasema: Basi malipo yake yatakuwa nini ikiwa nyinyi ni
waongo?
75. Wakasema: Malipo yake ni yule ambaye ataonekana nalo yeye huyo
ndiye malipo yake. Hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu.
76. Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha
akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza
kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu.
Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye
zaidi.
77. Wakasema: Ikiwa huyu ameiba, basi nduguye vile vile aliiba
zamani. Lakini Yusuf aliyaweka siri moyoni mwake wala hakuwaonyesha.
Akawaambia: Nyinyi mko katika hali mbaya zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi
hayo mnayo singizia.
78. Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo
mchukue mmoja wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu
wema.
79. Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipo
kuwa tuliye mkuta naye kitu chetu. Hivyo basi tutakuwa wenye kudhulumu.
80. Walipo kata tamaa naye wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao
akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kwenu kutokana na
Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo mlimkosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi
mimi sitotoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu
anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu.
81. Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Mwanao ameiba.
Na sisi hatutoi ushahidi ila kwa tunayo yajua. Wala sisi hatukuwa wenye
kuhifadhi mambo ya ghaibu.
82. Na waulize watu wa mji tulio kuwako, na msafara tulio kuja nao.
Na hakika sisi tunasema kweli.
83. Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani.
Subira ni njema! Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ni
Mjuzi Mwenye hikima.
84. Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Masikini Yusuf! Na macho
yake yakawa meupe kwa huzuni aliyo kuwa akiizuia.
85. Wakasema: Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au
uwe katika walio hiliki.
86. Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu
na huzuni yangu. Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi.
87. Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate
tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi
Mungu isipo kuwa watu makafiri.
88. Basi walipo ingia kwa Yusuf walisema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata
shida, sisi na watu wetu. Na tumeleta mali kidogo. Basi tupimie kipimo na fanya
kama unatupa sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.
89. Akasema: Je! Mmejua mliyo mfanyia Yusuf na nduguye mlipo kuwa
wajinga?
90. Wakasema: Kumbe wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na
huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anaye mcha Mungu
na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa wafanyao mema.
91. Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko
sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.
92. Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu
atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu.
93. Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa
mwenye kuona. Na mje nao watu wenu wote wa nyumbani.
94. Na ulipo ondoka tu msafara baba yao alisema: Hakika mimi nasikia
harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu.
95. Wakasema: Wallahi! Hakika bado ungali katika upotovu wako wa
zamani.
96. Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea
kuona. Akasema: Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua
nyinyi?
97. Wakasema: Ee baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hapana
shaka sisi tulikuwa na makosa.
98. Akasema: Nitakuja kuombeeni msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika
Yeye ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kusamehe.
99. Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema:
Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani.
100. Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote
wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile
ndoto yangu ya zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. Na Mwenyezi
Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, na kukuleteni kutoka jangwani baada ya
Shet'ani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole
kwa alitakalo. Bila ya shaka Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
101. Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza
tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika
dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao
mema.
102. Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa
pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua
vitimbi.
103. Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi..
104. Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya ila ni mawaidha
kwa walimwengu wote.
105. Na ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazo zipitia, na hali
ya kuwa wanazipuuza.
106. Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni
washirikina.
107. Je! Wanaaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ya
kuwagubika, au haitawafikia Saa ya Kiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?
108. Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa
kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si
katika washirikina.
109. Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipo kuwa wanaume tulio
wafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je! Hawatembei katika ardhi
wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya
Akhera ni bora kwa wamchao Mungu. Basi hamfahamu?
110. Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa,
hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha
kaumu ya wakosefu.
111. Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Si
maneno yaliyo zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa
kila kitu, na ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini.