13 - AR-RAA'D
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Alif Lam Mym Ra. (A.L.M.R.) Hizi ni
Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola
wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu
hawaamini.
2. Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona,
ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja
kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na
Mola wenu Mlezi.
3. Na ndiye aliye itandaza ardhi na
akaweka humo milima na
4. Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, na zipo bustani
za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na
isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Na tunaifanya
baadhi
5. Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Ati
tukisha kuwa mchanga kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio walio mkufuru
Mola wao Mlezi. Na hao ndio watao kuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu
wa Motoni. Humo watadumu.
6. Na wanakuhimiza ulete maovu kabla ya mema, hali ya kuwa
zimekwisha pita kabla
7. Na wale walio kufuru husema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka
kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa
kuwaongoa.
8. Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila mwanamke, na kinacho
punguka na kuzidi matumboni. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.
9. Yeye ndiye Mwenye kujua yanayo onekana na yasio onekana; Mkuu
Aliye tukuka.
10. Ni sawa anaye ficha kauli yake kati yenu na anaye idhihirisha,
na anaye jibanza usiku na anaye tembea jahara mchana.
11. Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake
linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko
kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo
watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala
yake.
12. Yeye ndiye anaye kuonyesheni umeme kwa khofu na tamaa, na
huyaleta mawingu mazito.
13. Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia,
kwa kumkhofu. Naye hupeleka mapigo ya radi yakampata amtakaye. Nao wanabishana
juu ya Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Mwenye adhabu kali!
14. Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake
hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji
ili yafike kinywani mwake, lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila
katika upotovu.
15. Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu
tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni.
16. Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi
Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao
hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa
sawa? Au hebu huwa sawa
17. Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji
kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na
kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea
povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na
baat'ili. Basi lile povu linapita
18. Walio muitikia Mola wao Mlezi watapata wema. Na wasio muitikia,
hata wangeli kuwa navyo vyote viliomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya
shaka wangeli vitoa kujikombolea! Hao watapata hisabu mbaya kabisa, na makao
yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahala pabaya mno!
19. Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola
wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanao
zingatia,
20. Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji
maagano.
21. Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na
wanaikhofu hisabu mbaya.
22. Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na
wakashika Sala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na
wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya
Akhera.
23. Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema
miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia
katika kila mlango.
24. (Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu
ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.
25. Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga,
na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika
nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.
26. Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa
kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na
Akhera si kitu ila ni starehe ndogo.
27. Na wanasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka
kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humwacha kupotea amtakaye, na
humwongoa anaye elekea kwake,
28. Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi
Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!
29. Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo
mazuri.
30. Ndio kama hivi tumekutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla
yao umati nyengine, ili uwasomee tunayo kufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani,
Mwingi wa Rehema! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hapana mungu isipo kuwa
Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndio marejeo yangu!
31. Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na
kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali
mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa
Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio
kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu
na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu
havunji miadi yake.
32. Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume walio kuwa kabla yako. Na
nikawapururia wale walio kufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!
33. Je! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyo yachuma...? Na
wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa
khabari ya yale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu? Bali walio kufuru
wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu
amemwacha apotee basi hana wa kumwongoa.
34. Wanayo adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera hapana
shaka ina mashaka zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi
Mungu.
35. Mfano wa Bustani waliyo ahidiwa wachamngu, kati yake inapita
mito, matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale
walio walio jilinda. Na mwisho wa makafiri ni Moto.
36. Na tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika
makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu
Mwenyezi Mungu, na wala nisimshirikishe. Kuendea kwake Yeye ndiyo ninaita, na
kwake Yeye ndio marejeo yangu.
37. Na ndio kama hivi tumeiteremsha Qur'ani kuwa ni hukumu kwa lugha
ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya kukujia ilimu hii, hutakuwa na
rafiki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu.
38. Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na
tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo
kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake.
39. Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya
hukumu zote iko kwake.
40. Na ikiwa tukikuonyesha baadhi ya tuliyo waahidi au tukakufisha
kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hisabu.
41. Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake?
Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi
wa kuhisabu.
42. Na walipanga walio kuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye
Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma kila nafsi. Na makafiri watajua ni
ya nani nyumba ya mwisho Akhera!
43. Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu
anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya
Kitabu.