2 - AL - BAQARA
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Alif Lam Mim.
2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa
wachamungu,
3. Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na
hutoa katika tuliyo wapa.
4. Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na
yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.
5. Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa
Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa.
6. Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini.
7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio
yao, na juu ya macho
8. Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku
ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.
9. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini,
lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.
10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.
Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo.
11. Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema:
12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.
13. Na wanapo ambiwa: Aminini kama walivyo amini watu. Husema:
Tuamini kama walivyo amini wapumbavu? Hakika wao ndio wapumbavu, lakini hawajui
tu.
14. Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo
kuwa peke
15. Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao
wakitangatanga ovyo.
16. Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu; lakini biashara yao
haikupata tija, wala hawakuwa wenye kuongoka.
17. Mfano wao ni kama mfano wa aliye koka moto, na ulipo tanda
mwangaza wake kote kote Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawawacha katika
giza, hawaoni.
18. Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.
19. Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina giza na radi na
umeme; wakawa wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, kwa
kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri.
20. Unakaribia umeme kunyakua macho
21. Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na
wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka.
22. (Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama
tandiko, na mbingu
23. Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi
leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi
Mungu, ikiwa mnasema kweli.
24. Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto
ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha.
25. Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata
mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema:
Haya ndiyo
26. Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio
wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa
Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi
Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini
hawapotezi ila wale wapotovu,
27. Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na
wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika
nchi; hao ndio wenye khasara.
28. Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu
akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake
mtarejeshwa?.
29. Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena
akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila
kitu.
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka
katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu
humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa
utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.
31. Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele
ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.
32. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa
kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima.
33. Akasema: Ewe Adam! Waambie majina yake. Basi alipo waambia
majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za
duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha?
34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote
isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
35. Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na
kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa
katika wale walio dhulumu.
36. Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika
waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika
ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda.
37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake
Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na
Mwenye kurehemu.
38. Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu,
basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu
39. Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakao
kuwa watu wa Motoni, humo watadumu.
40. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni,
na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi
tu.
41. Na aminini niliyo yateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo,
wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo. Na
niogopeni Mimi tu.
42. Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi
mnajua.
43. Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na inameni pamoja na wanao
inama.
44. Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali
nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii?
45. Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika
jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu,
46. Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi na ya
kuwa hakika watarejea kwake.
47. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo
kuneemesheni, na nikakuteuweni kuliko wote wengineo.
48. Na iogopeni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote, wala
hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake; wala
hawatanusuriwa.
49. Na vile tulipo kuokoeni kwa watu wa Firauni walio kupeni adhabu
mbaya, wakiwachinja wana wenu wa kiume na wakawawacha hai wanawake; na katika
hayo ulikuwa ni mtihani mkubwa ulio toka kwa Mola wenu Mlezi.
50. Na tulipo ipasua bahari kwa ajili yenu na tukakuokoeni,
tukawazamisha watu wa Firauni, na huku mnatazama.
51. Na tulipo muahidi Musa masiku arubaini, kisha mkachukua ndama
(mkamuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu.
52. Kisha tukakusameheni baada ya hayo, ili mpate kushukuru.
53. Na tulipo mpa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka.
54. Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi
mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama (kumuabudu). Basi tubuni kwa
Muumba wenu na ziueni nafsi zenu. Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Naye
akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba na Mwenye kurehemu.
55. Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi
Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia.
56. Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu, ili mpate kushukuru.
57. Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna
na Salwa; tukakwambieni: Kuleni vitu vizuri hivi tulivyo kuruzukuni. Nao
hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao.
58. Na tulipo sema: Ingieni mji huu, na humo mle mpendapo maridhawa,
na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe!
Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia wema wafanyao wema.
59. Lakini walio dhulumu waliibadili kauli isiyo kuwa waliyo ambiwa.
Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale walio dhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa
sababu ya walivyo kuwa wamepotoka.
60. Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia:
Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila
kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya
Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.
61. Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna
moja tu, basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi,
kama mboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesi zake, na vitunguu
vyake. Akasema: Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko
mtapata mlivyo viomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini, na wakastahili
ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno
ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwa walivyo asi na
wakapindukia mipaka.
62. Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote
atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata
malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala
hawatahuzunika.
63. Na tulipo chukua ahadi yenu, na tukaunyanyua mlima juu yenu
(tukakwambieni): Shikeni kwa nguvu haya tuliyo kupeni, na yakumbukeni yaliyomo
ndani yake ili mpate kujilinda.
64. Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi
Mungu juu yenu na rehema zake, mngeli kuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.
65. Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja
Sabato,(siku ya mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani
wadhalilifu.
66. Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale walio kuwa katika
zama zao na walio kuja baada yao, na mawaidha kwa wachamngu.
67. Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu
anakuamrisheni mchinje ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema:
Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga.
68. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni ng'ombe
gani? Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba ng'ombe huyo si mpevu, wala si kinda,
bali ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyo amrishwa.
69. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie nini rangi yake?
Akasema: Yeye anasema, kuwa ng'ombe huyo ni wa manjano, na rangi yake imekoza,
huwapendeza wanao mtazama.
70. Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi?
Hakika tunaona ng'ombe wamefanana. Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu
akipenda, tutaongoka.
71. Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni ng'ombe asiye tiwa kazini
kulima ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta
haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo.
72. Na mlipo muuwa mtu, kisha mkakhitalifiana kwayo, na Mwenyezi
Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyo kuwa mkiyaficha.
73. Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo ng'ombe). Ndivyo hivi
Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate
kufahamu.
74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama
mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine
yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya
khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya.
75. Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia
maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na
hali wanajua?
76. Na wanapo kutana na wale walio amini husema: Tumeamini. Na
wanapo kuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyo kufunulieni
Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu
nyinyi?
77. Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na
wanayo yatangaza?
78. Na wako miongoni mwao wasio jua kusoma; hawakijui Kitabu isipo
kuwa uwongo wanao utamani, nao hawana ila ni kudhania tu.
79. Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema:
Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao
kwa yale iliyo andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma.
80. Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema:
Mmechukua ahadi kwa Mwenyezi Mungu? Kweli Mwenyezi Mungu hatokwenda kinyume na
ahadi yake. Au mnamsingizia Mwenyezi Mungu mambo msiyo yajua?
81. Naam, anaye chuma ubaya - na makosa yake yakamzunguka - hao ndio
watu wa Motoni; humo watadumu.
82. Na wale walio amini na wakatenda mema, hao ndio watu wa Peponi,
humo watadumu.
83. Na tulipo funga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila
Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini, na
semeni na watu kwa wema, na shikeni Sala, na toeni Zaka. Kisha mkageuka isipo
kuwa wachache tu katika nyinyi; na nyinyi mnapuuza.
84. Na tulipo chukua agano lenu kuwa hamtamwaga damu zenu, wala
hamtatoana majumbani mwenu; nanyi mkakubali nanyi mnashuhudia.
85. Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu
majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka
mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na
mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila
hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu
kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo
yatenda.
86. Hao ndio walio nunua uhai wa dunia kwa (uhai wa) Akhera; kwa
hivyo hawatapunguziwa adhabu wala hawatanusuriwa.
87. Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume
wengine. Na tukampa Isa, mwana wa Mariamu, hoja zilizo waziwazi, na tukamtia
nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipo kufikieni Mitume kwa yale ambayo
hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine
mkawauwa.
88. Na walisema: Nyoyo zetu zimefunikwa.
89. Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho
thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda
makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya
Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!
90. Kiovu kweli walicho jiuzia nafsi zao, nacho ni kule kukataa kwao
aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kuona maya kwa kuwa Mwenyezi
Mungu humteremshia fadhila yake amtakaye miongoni mwa waja wake. Basi
wamejiletea wenyewe ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata mateso ya
kudhalilisha.
91. Na wanapo ambiwa: Yaaminini aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Wao
husema: Tunaamini tuliyo teremshiwa sisi. Na huyakataa yasiyo kuwa hayo. Na
hali ya kuwa hii ndiyo Haki inayo thibitisha yale waliyo nayo wao. Sema: Mbona
mliwauwa Manabii wa Mwenyezi Mungu hapo zamani ikiwa kweli mlikuwa
Waumini?
92. Na alikufikieni Musa na hoja zilizo waziwazi, kisha mkamchukua
ndama (kumuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu.
93. Na tulipo chukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu
(tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya tuliyo kupeni na sikieni. Wakasema:
Tumesikia na tumekataa! Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa
kufuru
94. Sema: Ikiwa nyumba ya Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu
tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti
95. Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale yaliyo tangulizwa
na mikono
96. Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya
kuishi, na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa
miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Mwenyezi
Mungu anayaona wanayo yatenda.
97. Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye
iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha
yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.
98. Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake
na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.
99. Hakika tumekuteremshia Ishara zilizo wazi na hapana wanao
zikataa ila wapotovu.
100. Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni
mwao kikaivunja?
101. Na alipo wajia Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwenye kuthibitisha
yale waliyo nayo, kundi moja miongoni mwa wale walio pewa Kitabu lilitupa
Kitabu cha Mwenyezi Mungu hicho nyuma ya migongo
102. Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su
leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru,
wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na
Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika
sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya
kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi
Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua
kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni
kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
103. Na lau kuwa wangeamini na wakaogopa, bila ya shaka malipo
yatokayo kwa Mwenyezi Mungu yange kuwa bora. Laiti wangeli kuwa wanajua!
104. Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni:
"Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu.
105. Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina
hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na Mwenyezi
Mungu humkusudia kumpa rehema yake ampendaye. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila
kubwa.
106. Ishara yoyote tunayo ifuta au tunayo isahaulisha tunailetea
iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni
Muweza wa kila kitu?
107. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ana ufalme wa mbingu na ardhi? Nanyi
hamna mlinzi wala msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
108. Au mnataka kumwomba Mtume wenu
109. Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange
kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi
uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na
wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Muweza wa kila kitu.
110. Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia
nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo
yafanya.
111. Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo.
Hayo ni matamanio
112. Sivyo hivyo! Yeyote anaye elekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu
naye ni mtenda mema, basi ana malipo yake kwa Mola wake Mlezi, wala haitakuwa
khofu juu
113. Na Mayahudi husema: Wakristo hawana lao jambo. Na Wakristo
husema: Mayahudi hawana lao jambo. Na ilhali wote wanasoma Kitabu hicho hicho
(Biblia). Na kadhaalika walisema wale wasio jua kitu mfano wa kauli
114. Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya
Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina
115. Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote
mnako elekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa
na Mjuzi.
116. Na ati wanasema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu!
Ametakasika na hayo.
117. Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapo
taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa.
118. Na walisema wale wasio jua kitu: Mbona Mwenyezi Mungu hasemi
nasi au zikatufikia Ishara. Kama hivyo walisema wale walio kuwa kabla
119. Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki uwe mbashiri, na mwonyaji. Na
wala hutaulizwa juu ya watu wa Motoni.
120. Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila
121. Wale tulio wapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao
ndio kweli wanakiamini. Na wanao kikataa basi hao ndio wenye kukhasiri.
122. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni,
na hakika Mimi nikakufadhilisheni kuliko wengineo wote.
123. Na iogopeni siku ambayo hatamfaa mtu mwenziwe kwa lolote, wala
hakitakubaliwa kwake kikomboleo, wala maombezi hayatamfaa, wala
hawatanusuriwa.
124. Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani,
naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu.
Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia
wenye kudhulumu.
125. Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Alkaaba) iwe pahala pa
kukusanyikia watu na pahala pa amani. Na alipo kuwa akisimama Ibrahim pafanyeni
pawe pa kusalia. Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa
ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao
inama na kusujudu.
126. Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji
wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na
Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha
nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahala pabaya mno pa kurejea.
127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile
Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi
Mjuzi.
128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na
pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia
za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee
Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye
Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi
yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na
hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.
131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena:
Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.
132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika
Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu,
wanyenyekevu.
133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe:
Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba
zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu
kwake.
134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi
mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya
wao.
135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema:
136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo
teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub
na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine
kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi
tumesilimu kwake.
137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli
wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu
atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.
138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora
wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.
139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu
Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo
vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.
140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu
zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi
Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio
nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo
myafanyayo.
141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na
nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa
wakifanya wao.
142. WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza
kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya
Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka.
143. Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe
mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla
ulicho kuwa nacho ila tupate kumjua yule anaye mfuata Mtume na yule anaye geuka
akarejea nyuma. Na kwa yakini
144. Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi
tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti
Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; na hakika
wale walio pewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi.
Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.
145. Na hao walio pewa Kitabu, hata ukiwaletea hoja za kila namna,
hawatafuata Kibla chako; wala wewe hutafuata kibla chao, wala baadhi yao
hawatafuata kibla cha wengineo; na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya
kukufikia ujuzi, hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhullumu.
146. Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya
147. Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao
fanya shaka.
148. Na kila mmoja anao upande anao elekea. Basi shindanieni mema.
Popote mlipo Mwenyezi Mungu atakuleteni nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Muweza wa kila kitu.
149. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na
hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye
kughafilika na mnayo yatenda.
150. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na
popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu,
isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni
Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.
151. Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana na nyinyi,
anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hikima na
kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui.
152. Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na nishukuruni wala
msinikufuru.
153. Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika
Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.
154. Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu
ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui.
155. Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na
upungufu wa
156. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi
Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.
157. Hao juu
158. Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi
Mungu. Basi anaye hiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake
kuvizunguka. Na anaye jitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu
ni Mwenye shukrani na Mjuzi.
159. Hakika wale wanao ficha tuliyo yateremsha -- nazo ni hoja zilizo
wazi na uwongofu baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu Kitabuni -- hao anawalaani
Mwenyezi Mungu, na wanawalaani kila wenye kulaani.
160. Ila wale walio tubu na wakatengeneza na wakabainisha, basi hao
nitapokea toba yao, na Mimi ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
161. Hakika walio kufuru na wakafa hali ni makafiri, hao iko juu
162. Watadumu humo. Hawata-punguziwa adhabu wala hawatapewa muda wa
kupumzika.
163. Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi
wa rehema, Mwenye kurehemu.
164. Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana
usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na
maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha
ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika
mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi,
bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.
165. Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi
Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda
Mwenyezi Mungu zaidi
166. Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya
kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano
167. Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa
wao
168. Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala
msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.
169. Yeye anakuamrisheni maovu na machafu, na mumsingizie Mwenyezi
Mungu mambo msiyo yajua.
170. Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao
husema:
171. Na mfano wa walio kufuru ni kama mfano wa anaye mpigia kelele
asiye sikia ila wito na sauti tu -- ni viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo
hawaelewi.
172. Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru
Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.
173. Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na
kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu.
Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana
dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
174. Hakika wale wafichao aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika
Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa
moto, wala Mwenyezi Mungu hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao
watapata adhabu chungu.
175. Hao ndio walio nunua upotofu badala ya uwongofu, na adhabu
badala ya maghfira. Ama wavumilivu wa Moto watu hawa!
176. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki.
Na wale walio khitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na
haki.
177. Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na
magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na
Malaika na Kitabu na Manabii, na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na
mayatima na masikini na wasafiri, na waombao, na katika ugombozi, na akawa
anashika Sala, na akatoa Zaka, na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi, na wanao
vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha, na
hao ndio wajilindao.
178. Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa
- muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na
anaye samehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye
alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kuliko tokana na Mola wenu Mlezi, na ni
rehema. Na atakaye vuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu
chungu.
179. Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili,
ili msalimike.
180. Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha
181. Na atakaye ubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake
ni juu ya wale watakao ubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia
Mwenye kujua.
182. Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi
akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Msamehevu na Mwenye kurehemu.
183. 183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu,
184. (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni
mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na
wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa
kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu,
185. Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni
uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye
kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi
atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi
wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi
Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.
186. Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi
nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi,
na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.
187. Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni
vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa
mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni.
Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na
kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa
usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali
mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie.
Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate
kumcha.
188. Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu
ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua.
189. Wanakuuliza khabarai ya miezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati
kwa ajili ya watu na Hija. Wala sio wema kuziingia nyumba kwa nyuma.
190. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni,
wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.
191. Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni;
kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti
Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na
hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.
192. Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
193. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi
Mungu tu. Na
194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu
vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo
kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu
pamoja na wachamngu.
195. Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono
yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda
wafanyao wema.
196. Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa
mkizuiwa,basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa
vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakaye kuwa mgonjwa au ana
vya kumuudhi kichwani mwake basi atoe fidiya kwa kufunga au kwa kutoa sadaka au
kuchinja wanyama. Na mtakapo kuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa
kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na
asiye pata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakapo rudi; hizi ni
kumi kaamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na
Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni Mwenyezi Mungu ni Mkali
wa kuadhibu.
197. Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika
miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala
asibishane katika Hija. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. Na
jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu. Na nicheni Mimi,
enyi wenye akili!
198. Si vibaya kwenu kuitafuta fadhila ya Mola wenu Mlezi. Na mtakapo
miminika kutoka A'rafat mtajeni Mwenyezi Mungu penye Masha'ril Haram. Na
mkumbukeni kama alivyo kuongoeni, ijapo kuwa zamani mlikuwa miongoni mwa walio
potea.
199. Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminika watu, na muombeni
Mwenyezi Mungu msamaha: hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
200. Na mkisha timiza ibada zenu basi mtajeni Mwenyezi Mungu
201. Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani
mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!
202. Hao ndio watakao pata sehemu
203. Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa.
Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake;
na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni
Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.
204. Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya
kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni
mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu.
205. Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na
kuteketeza mimea na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.
206. Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa
kutenda madhambi. Basi huyo inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa
mapumziko.
207. Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za
Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake.
208. Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala
msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.
209. Na ikiwa mkateleza baada ya kukufikieni hoja zilizo wazi, basi
jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
210. Je wanangoja mpaka Mwenyezi Mungu awajie katika vivuli vya
mawingu pamoja na Malaika, na hukumu iwe imekwisha tolewa? Na kwa Mwenyezi
Mungu ndio hurejeshwa mashauri yote.
211. Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi? Na
anaye zibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia basi hakika Mwenyezi
Mungu ni mkali wa kuadhibu.
212. Walio kufuru wamepambiwa maisha ya duniani; na wanawafanyia
maskhara walio amini. Na wenye kuchamngu watakuwa juu
213. Watu wote walikuwa ni umma mmoja. Mwenyezi Mungu akapeleka
Manabii wabashiri na waonyaji. Na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa Haki, ili
kihukumu baina ya watu katika yale walio khitalifiana. Na wala
hawakukhitalifiana ila wale walio pewa Kitabu hicho baada ya kuwafikia hoja
zilizo wazi, kwa sababu ya uhasidi baina
214. Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni
215. Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya
wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo
ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.
216. Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda
mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari
kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.
217. Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema:
Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasende katika
Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye
Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi
Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala hawatoacha kupigana nanyi
mpaka wakutoeni katika Dini yenu
218. Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia
ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
219. Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo
dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko
manufaa yake. Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi
Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri--
220. --katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Na wanakuuliza juu
ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio kheri. Na mkichanganyika nao basi ni
ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi
Mungu angeli penda angeli kutieni katika udhia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye
nguvu na Mwenye hikima.
221. Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi
Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti
zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora
kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi
Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya
zake kwa watu ili wapate kukumbuka.
222. Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi
jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike.
Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha.
223. Wake zenu ni
224. Wala msifanye jina la Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa ni
kisingizio cha kuacha kufanya wema na kuchamngu na kupatanisha baina ya watu.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
225. Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi.
226. Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine.
Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye
kurehemu.
227. Na wakiazimia kuwapa talaka basi, Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kusikia na Mjuzi.
228. Na wanawake walio achwa wangoje peke
229. T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa
vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlicho wapa wake zenu, ila ikiwa
wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi
Mungu. Basi mkiogopa kuwa hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu
hapo itakuwa hapana lawama ikiwa mwanamke atajikomboa. Hii ndiyo mipaka ya
Mwenyezi Mungu; basi msiikiuke. Na watakao ikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao
ndio madhaalimu.
230. Na
231. Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikia kumaliza eda
yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa
kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala
msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya
Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anacho
kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi
Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
232. Na mtakapo wapa wanawake t'alaka nao wakamaliza eda yao, basi
msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina
233. Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili
kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama,
na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo
wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya
mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka
kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka
kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa
mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba
Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.
234. Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake
wangoje peke
235. Wala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa
wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua
kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema.
Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba
Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi tahadharini naye. Na
jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.
236. Hapana ubaya kwenu mkiwapa t'alaka wanawake ambao hamjawagusa au
kuwabainishia mahari
237. Na mkiwapa t'alaka kabla ya kuwagusa, na mmekwisha wawekea hayo mahari
makhsusi, basi wapeni nusu ya mahari mlio agana, isipo kuwa ikiwa wanawake
wenyewe wamesamehe, au mume ambaye kifungo cha ndoa ki mikononi mwake awe
amesamehe. Na kusameheana ndiko kulio karibu zaidi na uchamngu. Wala msisahau
fadhila baina yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
238. Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili
ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).
239. Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda.
Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu
240. Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakawacha wake, na wausie
kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa nyumba.
Na wanawake wenyewe wakiondoka, basi hapana ubaya kwenu kwa waliyo jifanyia
wenyewe kwa mujibu wa Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye
hikima.
241. Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa mujibu wa
Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu.
242. Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate
kufahamu.
243. Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa
mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akwahauisha. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.
244. Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba
Mwenyezi Mungu ni Msikizi na Mjuzi.
245. Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili
amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake
Yeye mtarejea.
246. Hukuwaona watukufu katika Wana wa Israili baada ya Musa, walipo
mwambia Nabii wao: Tuwekee mfalme ili tupigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu?
Akasema: Je, haielekei ikiwa mtaandikiwa vita kuwa msipigane? Wakasema:
Itakuwaje tusipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na hali tumetolewa
majumbani kwetu na watoto wetu? Lakini walipo andikiwa kupigana waligeuka,
isipo kuwa wachache miongoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu.
247. 247, Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Mungu amekuteulieni Taluti
(Sauli) kuwa ni mfalme. Wakasema: vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi
tuna haki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa
248. Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni
lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu
Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Harun, wanalichukua
Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini.
249. Basi Taluti alipo ondoka na majeshi alisema: Mwenyezi Mungu
atakujaribuni kwa mto. Atakaye kunywa humo si pamoja nami, na asiye kunywa
atakuwa pamoja nami: ila atakaye teka kiasi ya kitanga cha mkono wake. Lakini
walikunywa humo isipo kuwa wachache tu miongoni mwao. Alipo vuka mto yeye na
wale walio amini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na
majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Makundi
mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na
Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
250. 250, Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema:
Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie
tuwashinde watu Makafiri--
251. --Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na Daudi akamuuwa
Jaluti, na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hikima, na akamfundisha aliyo
yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia
ingeli haribika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu
wote.
252. Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na hakika
wewe ni miongoni mwa Mitume.
253. MITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao
wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na
tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu.
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada
ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio
amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda
wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.
254. Enyi mlio amini! Toeni katika tulivyo kupeni kabla haijafika
Siku ambayo hapatakuwapo biashara, wala urafiki, wala uombezi. Na makafiri ndio
madhaalimu.
255. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo
yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo
mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini
yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika
vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni
na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na
ndiye Mkuu.
256. Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha
pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu
bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu
ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
257. Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na
kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa
kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo
watadumu.
258. Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi
kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule
ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim
akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe
magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu
madhaalimu.
259. Au kama yule aliye pita karibu na mji ulio kwisha kuwa magofu
tu, akasema: Ataufufuaje Mwenyezi Mungu mji huu baada ya kufa kwake? Basi
Mwenyezi Mungu alimfisha yeye muda wa miaka mia. Kisha akamfufua. Akamuuliza:
Je umekaa muda gani? Akajibu: Labda nimekaa siku moja au sehemu ya siku.
Akamwambia: Bali umekaa miaka mia wewe. Hebu angalia chakula chako na vinywaji
vyako, havikuharibika. Na muangalie punda wako. Na ili tukufanye uwe ni Ishara
kwa watu iangalie hii mifupa yake jinsi tunavyo inyanyua kisha tunaivisha
nyama. Basi yalipo mbainikia alinena: Najua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye
uweza juu ya kila kitu.
260. Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyo
fufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili
moyo wangu utue. Akamwambia: Twaa ndege wane na uwazoeshe kwako, kisha uweke
juu ya kila kilima sehemu, kisha wete, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika
Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.
261. Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni
kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo
punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye
wasaa na Mwenye kujua.
262. Wanao toa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha
hawafuatishii masimbulizi wala udhia kwa walicho toa, wana ujira wao kwa Mola
wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.
263. Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa
na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole.
264. Enyi mlio amini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na
maudhi, kama anaye toa mali yake kwa kuwaonyesha watu, wala hamuamini Mwenyezi
Mungu wala Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama mfano wa jabali ambalo juu
yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa, ikaliacha tupu. Basi
hawatakuwa na uweza wowote kwa walivyo chuma. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu
makafiri.
265. Na mfano wa wale wanao toa mali zao kwa kuitafuta radhi ya
Mwenyezi Mungu na kuzipa nguvu roho zao ni kama mfano wa bustani iliyo mahali
pa juu, ikaifikia mvua kubwa na ikaleta mazao yake mardufu; na hata kama
haifikiwi na mvua kubwa basi manyunyu hutosha. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo
yatenda.
266. Je! Yupo mmoja wenu anaye penda kuwa na kitalu cha mitende na
mizabibu ipitayo mito kati yake, naye humo hupata mazao ya kila namna, na uzee
ukamfikia naye hali ana watoto wanyonge, kikapigwa na kimbunga chenye moto,
kikaungua? Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Ishara ili mpate
kufikiri.
267. Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na
katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo
vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na
jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.
268. Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo
machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.
269. Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka
amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili.
270. Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika
Mwenyezi Mungu anajua. Na walio dhulumu hawana wa kuwanusuru.
271. Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri
kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na
Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
272. Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa
amtakaye. Na kheri yoyote mnayo toa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa
kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mtakayo toa mtalipwa kwa
ukamilifu, wala hamtadhulumiwa.
273. Nawapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu,
wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiye wajua hali zao
huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama
zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Na kheri yoyote mnayo toa, basi kwa
yakini Mwenyezi Mungu anaijua.
274. Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri,
wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala
hawatahuzunika.
275. Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na
Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini
Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa
na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo
kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao
ndio watu wa Motoni, humo watadumu.
276. Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na
Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.
277. Hakika wale walio amini na wakatenda mema na wakashika Sala na
wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu
juu yao, wala hawatahuzunika.
278. Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo
bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.
279. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume
wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala
msidhulumiwe.
280. Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike.
Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua.
281. Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha
kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.
282. Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi
andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae
kuandika. Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake
aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze
chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au
hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na
mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili,
basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi.
Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi
wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka
muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi
kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya
mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini
mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na
mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
283. Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa
rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe
amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala msifiche
ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayo yatenda.
284. Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na
mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu
atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi
Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
285. Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi
wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake,
na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume
wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola
Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.
286. Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya
iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu
yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola
wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu.
Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na
uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya
makafiri.