39 - AZZUMAR
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Mteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye
nguvu, Mwenye hikima.
2. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa
Haki. Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu.
3. Hakika Dini
4. Lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka kuwa na mwana, basi bila ya
shaka angeli teua amtakaye katika alio waumba. Subhanahu, Ametakasika na hayo!
Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo.
5. Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana,
na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila
kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye
Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe!
6. Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe
katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni
katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye
Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye.
Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
7. Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini
hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala
mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi.
Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema
yaliyomo vifuani.
8. Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye
ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa
akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia
yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa
miongoni mwa watu wa Motoni.
9. Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama
akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Ati
watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu
wenye akili.
10. Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale
wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu.
Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.
11. Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu kwa
kumsafishia Dini Yeye tu.
12. Na nimeamrishwa niwe wa mwanzo wa Waislamu.
13. Sema: Hakika mimi ninaogopa adhabu ya Siku Kubwa nikimuasi Mola
wangu Mlezi.
14. Sema: Mwenyezi Mungu tu namuabudu kwa kumsafishia Yeye tu Dini
yangu.
15. Basi nyinyi abuduni mpendacho badala yake Yeye. Sema: Hakika
walio khasirika ni wale walio jikhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama.
Tambueni kuwa hiyo ndiyo khasara iliyo dhaahiri.
16. Yatawekwa juu yao mat'abaka ya moto, na chini
17. Na wale wanao jiepusha na ibada potovu, na wakarejea kwa
Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu.
18. Ambao husikiliza maneno, wakafuata lilio bora
19. Je! Yule mwenye kustahiki hukumu ya adhabu, je, wewe unaweza
kumwokoa aliyomo katika Moto?
20. Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizo jengwa
juu ya ghorofa; chini yake hupita
21. Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka
mbinguni. Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa maji hayo
akatoa mimea yenye rangi mbali mbali? Kisha hunyauka ukaiona imekuwa kimanjano,
na kisha huifanya mapepe. Bila ya shaka katika hayo upo ukumbusho kwa wenye
akili.
22. Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa
Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na
mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi
Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri.
23. Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye
kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao
Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu.
Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye
ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa.
24. Je! Atakaye kuwa anapambana kwa uso wake na adhabu mbaya kabisa
Siku ya Kiyama (ni sawa na watenda wema?) Na wataambiwa wenye kudhulumu: Onjeni
hayo mliyo kuwa mkiyachuma!
25. Walio kuwa kabla yao walikadhibisha , na ikawajia adhabu kutoka
pahala wasipo patambua.
26. Basi Mwenyezi Mungu akawaonjesha hizaya katika uhai wa duniani.
Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi; laiti wangeli jua!
27. Na bila ya shaka tumewapigia watu mifano ya kila namna katika
hii Qur'ani ili wapate kukumbuka.
28. Qur'ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu.
29. Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika
wanao gombana, na wa mtu mwengine aliye khusika na bwana mmoja tu. Je! Wako
sawa katika hali zao? Alhamdulillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu!
Lakini wengi wao hawajui.
30. Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa.
31. Kisha bila ya shaka mtagombana Siku ya Kiyama mbele ya Mola wenu
Mlezi.
32. BASI NI NANI dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye msingizia uwongo
Mwenyezi Mungu na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Siyo katika Jahannamu makaazi
ya hao makafiri?
33. Na aliye ileta Kweli na akaithibitisha - hao ndio wachamngu.
34. Watapata watakacho taka kwa Mola wao Mlezi. Hayo ndiyo malipo ya
watendao mema.
35. Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu walio ufanya na
awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema walio kuwa wakiutenda.
36. Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati
wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi
Mungu kupotea hana wa kumwongoa.
37. Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa hana wa kumpotoa. Je!
Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anaye weza kulipiza?
38. Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi. Bila ya
shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya
Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea
dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema:
Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea.
39. Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni mwezavyo, mimi pia nafanya. Basi
mtakuja ona
40. Ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mshukia
adhabu ya daima.
41. Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa
Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka
amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao. *
42. MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa
wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine
mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa
watu wanao fikiri.
43. Au ndio wanachukua waombezi badala ya Mwenyezi Mungu? Sema:
Ingawa hawana mamlaka juu ya kitu chochote, wala hawatambui lolote?
44. Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu
ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake.
45. Na anapo tajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasio iamini
Akhera huchafuka. Na wanapo tajwa wenginewe asiye kuwa Yeye basi wao
hufurahi.
46. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Muumba mbingu na ardhi! Mjuzi wa
yasiyo onekana na yanayo onekana! Wewe utahukumu baina ya waja wako katika
waliyo kuwa wakikhitalifiana.
47. Na lau kuwa walio dhulumu wangeli kuwa na vyote viliomo duniani
na pamoja navyo vingine kama hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikomboa
katika adhabu mbaya hiyo Siku ya Kiyama. Na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu
wasiyo kuwa wakiyatarajia.
48. Na utawadhihirikia ubaya wa waliyo yachuma, yatawazunguka waliyo
kuwa wakiyafanyia mzaha.
49. Na dhara inapo mgusa mtu hutuomba. Kisha tunapo mpa neema
zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya kwa sababu ya ilimu yangu. Sio! Huo ni
mtihani! Lakini wengi wao hawajui!
50. Waliyasema haya waliyo kuwa kabla yao, lakini hayakuwafaa waliyo
kuwa wakiyachuma.
51. Basi ukawasibu uovu wa waliyo yachuma. Na wale walio dhulumu
miongoni mwa hawa utawasibu uovu wa waliyo yachuma vile vile. Nao si wenye
kushinda.
52. Kwani wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki
amtakaye na akamkadiria? Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu
wanao amini.
53. Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa
na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika
Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
54. Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya
kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa.
55. Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyo teremshwa kwenu
kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali
hamtambui.
56. Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyo poteza
upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanao fanya
maskhara!
57. Au ikasema: Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka
ningeli kuwa miongoni mwa wenye kumchamngu.
58. Au ikasema inapo ona adhabu: Lau kuwa ningeli pata fursa
nyengine, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema.
59. Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe
ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri!
60. Na Siku ya Kiyama utawaona walio msingizia uwongo Mwenyezi Mungu
nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanao takabari?
61. Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu
kwao. Hapana uovu utao wagusa, wala hawatahuzunika.
62. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi
juu ya kila kitu.
63. Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale walio zikataa
Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kukhasiri.
64. Sema: Je! Mnaniamrisha nimuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, enyi
majaahili?
65. Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako:
Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima
utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri.
66. Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye
kushukuru.
67. Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri
yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa
katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa'la Ametakasika na Ametukuka na
hayo wanayo mshirikisha nayo.
68. Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo
katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara
nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea.
69. Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu
kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa
haki, wala hawatadhulumiwa.
70. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyo yafanya, na Yeye anayajua
sana wanayo yatenda.
71. Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka
watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani
hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na
kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti
neno la adhabu juu ya makafiri.
72. Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni
ubaya ulioje wa makaazi ya wanao takabari!
73. Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa
makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi
wake watawaambia: Salaam Alaikum, Amani iwe juu yenu! Mmet'ahirika. Basi
ingieni humu mkae milele.
74. Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi
Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani
popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!
75. Na utawaona Malaika wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha
Mwenyezi Mungu, wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi. Na patahukumiwa baina
yao kwa haki na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa
viumbe vyote!