45 - AL - JAATHIYA
KWA JINA
LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. H'a Mim
2. Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
3. Hakika katika mbingu na ardhi ziko
Ishara kwa Waumini.
4. Na katika umbo lenu na katika wanyama
alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye yakini.
5. Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo
iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya
kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.
6. Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa
haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya
zake?
7. Ole wake kila mzushi mwenye dhambi!
8. Anaye sikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia
yale yale aliyo katazwa, na anajivuna,
9. Na anapo kijua kitu kidogo katika Aya zetu hukifanyia mzaha.
Watu hao ndio watakao kuwa na adhabu ya kufedhehesha.
10. Na nyuma
11. Huu ni uwongofu. Na wale wale walio zikataa Ishara za Mola wao
Mlezi watapata adhabu inayo tokana na ghadhabu iliyo chungu.
12. Mwenyezi Mungu ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo
zipite marikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate
kushukuru.
13. Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika
ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao
fikiri.
14. Waambie walio amini wawasamehe wale wasio zitaraji siku za
Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma.
15. Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye
kutenda uovu ni juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.
16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii,
na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu
wote.
17. Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakukhitalifiana ila
baada ya kuwajia ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliyo kuwa baina
18. Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate,
wala usifuate matamanio ya wasio jua kitu.
19. Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika
wenye kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa
wamchao.
20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na
rehema kwa watu wanao yakinisha.
21. Je! Wanadhani wanao tenda maovu kuwa tutawafanya kama walio
amini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya
wanayo ihukumu!
22. Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili
kila nafsi ilipwe yale iliyo yachuma. Nao hawatadhulumiwa.
23. Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake,
na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri
juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi
nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
24. Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na
twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu
ya hayo, ila wao wanadhani tu.
25. Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema:
Waleteni baba zetu, ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.
26. Sema: Mwenyezi Mungu anakuhuisheni, kisha anakufisheni, kisha
anakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.
27. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na
siku itapo simama Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na
upotovu.
28. Na utauona kila umma umepiga magoti, na kila umma utaitwa kwenda
soma kitabu chake: Leo mtalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.
29. Hichi kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi
tulikuwa tukiyaandika mliyo kuwa mkiyatenda.
30. Ama walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia
katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi.
31. Na ama walio kufuru, wataambiwa: Kwani hamkuwa mkisomewa Aya
zangu nanyi mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu?
32. Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa
haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala
hatuna yakini.
33. Basi ubaya wa waliyo yatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka
waliyo yafanyia maskhara.
34. Na itasemwa: Leo tunakusahauni kama nyinyi mlivyo sahau mkutano
wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kukunusuruni.
35. Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu;
na maisha ya dunia yakakudanganyeni. Basi leo hawatatolewa humo wala hao
hawatakubaliwa udhuru wao.
36. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu,
na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
37. Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni
Mwenye nguvu, Mwenye hikima.