47 - MUH'AMMAD
KWA JINA
LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.
2. Na walio amini, na wakatenda mema, na
wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao
Mlezi - atawafutia makosa
3. Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio
amini wamefuata Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu
anavyo wapigia watu mifano
4. Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka
mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe,
mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda
mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na
walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
5. Atawaongoza na awatengezee hali
6. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha.
7. Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na
ataithibitisha miguu yenu.
8. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo
vyao.
9. Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu,
basi akaviangusha vitendo vyao.
10. Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa
walio kuwa kabla
11. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na
makafiri hawana mlinzi.
12. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema
katika Bustani zipitiwazo na
13. Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu
ulio kutoa; nao tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru.
14. Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama
aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao?
15. Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo
vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye
ladha kwa wanywao, na
16. Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako
huwauliza walio pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi
Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.
17. Na wale walio ongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamngu
wao.
18. Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa
ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi
kukumbuka hapo?
19. Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba
maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi
Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
20. Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo
teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye
maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni
bora kwao
21. Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni
wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni kheri kwao.
22. Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na
mwatupe jamaa zenu?
23. Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na
akawapofoa macho
24. Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo
kufuli?
25. Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu,
Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.
26. Hayo ni kwa sababu waliwaambia walio chukia aliyo yateremsha
Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua
siri zao.
27. Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso
zao na migongo yao!
28. Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi
Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.
29. Je! Wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu
hatazidhihirisha chuki zao?
30. Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa
alama zao; lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi
Mungu anavijua vitendo vyenu.
31. Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapignao Jihadi
katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu.
32. Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na
wakapinzana na Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru
Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
33. Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, wala
msiviharibu vitendo vyenu.
34. Hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha
wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao.
35. Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda.
Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo
vyenu.
36. Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamchamngu
Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hakutakeni mali yenu.
37. Na akikutakeni hayo na kukushikilieni mtafanya ubakhili, na
atatoa undani wa chuki zenu.
38. Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu,
na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi
anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio
wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama
nyinyi.