50 - QAAF
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!
2. Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni
mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu!
3. Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!
4. Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi
kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.
5. Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika
mambo ya mkorogo.
6. Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu
7. Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea
mizuri ya kila namna.
8. Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye
kuelekea.
9. Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa
hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.
10. Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi,
11.
12. Kabla
13. Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i.
14. Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao
waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu
15. Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza.
16. Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika
nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
17. Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na
kushotoni.
18. Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
19. Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo
kuwa ukiyakimbia.
20. Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
21. Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.
22. (Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo
tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali.
23. Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha
tayarishwa.
24. Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda,
25. Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka,
26. Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni
katika adhabu kali.
27. Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye
mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali.
28. (Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni
mbele onyo langu.
29. Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja
wangu.
30. Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna
ziada?
31. Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa
mbali.
32. Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi
Mungu na akajilinda.
33. Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja
kwa moyo ulio elekea-
34. (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima
dawamu.
35. Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
36. Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla
37. Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega
sikio naye yupo anashuhudia.
38. Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina
yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu.
39. Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako
Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
40. Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
41. Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala
karibu.
42. Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya
kufufuka.
43. Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio
marejeo.
44. Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni
mwepesi.
45. Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa
ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo.