54 - AL-QAMAR
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Saa imekaribia, na mwezi
umepasuka!
2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na
husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio
4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo
linalo chusha;
7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio
tawanyika,
8. Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku
ngumu.
9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na
wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi
nimeshindwa, basi ninusuru!
11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo
miminika.
12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo
lilio kadiriwa.
13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa
amekanushwa.
15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye
kumbuka?
16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika.
Lakini yupo anaye kumbuka?
18. Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo
yangu?
19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi
mfululizo,
20. Ukiwang'oa watu
21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika;
lakini yupo anaye kumbuka?
23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo
sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote?
26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame
tu na ustahamili.
28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina
29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa
32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa
kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
33. Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa
wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye
shukuru.
36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka
hayo maonyo.
37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na
tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
40. Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye
kumbuka?
41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo
shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni
kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na
chungu zaidi.
47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso
wa Jahannamu!
49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo
anaye kumbuka?
52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.