58 - AL - MUJAADALAH
KWA JINA
LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. MWENYEZI MUNGU amekwisha sikia usemi wa mwanamke anaye jadiliana
nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu
anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye
kuona.
2. Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao.
Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Na hakika hao wanasema neno linalo
chusha, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye
kusamehe.
3. Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale
waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa
hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.
4. Na asiye pata mtumwa kumkomboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo
kabla hawajagusana. Na asiye weza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni
hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya
Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri iko adhabu chungu.
5. Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake,
watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla
6. Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyo
yatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye kushuhudia kila kitu.
7. Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu
na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane
wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao,
wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku
ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila
kitu.
8. Kwani huwaoni wale walio katazwa kunong'onezana kisha
wakayarudia yale yale waliyo katazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi,
na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia hukuamkia sivyo anavyo kuamkia
Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya
tuyasemayo? Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo
maovu yaliyoje!
9. Enyi mlio amini! Mnapo nong'ona msinong'one kwa sababu ya mambo
ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezane kwa kutenda mema na
kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote.
10. Kwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe
walio amini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na
juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.
11. Enyi mlio amini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi
fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa:
Ondokeni, basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua walio amini miongoni mwenu,
na walio pewa ilimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo
yatenda.
12. Enyi mlio amini! Mnapo sema siri na Mtume, basi tangulizeni
sadaka kabla ya kusemezana kwenu. Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa
hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye
kurehemu.
13. Mnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu?
Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi shikeni Sala,
na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo
khabari za mnayo yatenda.
14. Huwaoni wale walio fanya urafiki na watu ambao Mwenyezi Mungu
amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uwongo,
na hali kuwa wanajua.
15. Mwenyezi Mungu amewaandalia adhabu kali. Kwa hakika waliyo kuwa
wakiyatenda ni maovu kabisa.
16. Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi
Mungu. Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
17. Hayatawafaa kitu mali yao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi
Mungu. Hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu milele. P>18. Siku atakayo wafufua
Mwenyezi Mungu wote, wamuwapie kama wanavyo kuwapieni nyinyi. Na watadhani kuwa
wamepata kitu! Kwa hakika hao ndio waongo.
18. 19. Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi
Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi la Shetani ndilo lenye
kukhasirika.
19. 20. Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio
miongoni mwa madhalili wa mwisho.
20. 21. Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu
tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.
21. 22. Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho
kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba
zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao
Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani
yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na
wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi
la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.