59 - AL - H'ASHRI
KWA JINA
LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Vinamsabihi, Vinamtakasa Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Naye ni
Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
2. Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza.
Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia, na akatia woga katika nyoyo
zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono
3. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeli waandikia kutoka, angeli
waadhibu katika dunia. Na katika Akhera watapata adhabu ya Moto.
4. Hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na
mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa
kuadhibu.
5. Mtende wowote mlio ukata au mlio uacha unasimama vile vile juu
ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuwahizi
wapotovu.
6. Na
7. Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa
hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na
mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu
miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni
jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa
kuadhibu.
8. Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao
kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na
wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli.
9. Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda
walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa
(Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni
wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye
kufanikiwa.
10. Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie
sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo
zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye
kurehemu.
11. Huwaoni wanao fanya unaafiki wanawaambia ndugu zao walio kufuru
katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala
hatutamt'ii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni.
Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo.
12. Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita
hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo; kisha
hawatanusuriwa.
13. Hakika nyinyi ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi
Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu kitu.
14. Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji
vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali.
Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa
wao ni watu wasio na akili.
15. Ni kama mfano wa walio kuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja
uovu wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu.
16. Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru
humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola
Mlezi wa walimwengu wote.
17. Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao ni kuingia Motoni, wadumu
humo daima; na hiyo ndiyo jaza ya madhaalimu.
18. Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie
inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi
Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.
19. Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye
akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio wapotovu.
20. Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi
ndio wenye kufuzu.
21. Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya
shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo
mifano tunawapigia watu ili wafikiri.
22. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye
tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa
rehema, Mwenye kurehemu.
23. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye
tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha
Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa,
Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.
24. Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye
majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni
Mwenye kushinda, Mwenye hikima.