6 -
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi,
na akafanya
2. Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni
ajali, na muda maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka.
3. Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na
ardhini. Anajua ya ndani yenu na ya nje yenu. Na anajua mnayo yachuma.
4. Na haiwafikii hata ishara moja katika ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa wenye kuipa nyongo.
5. Wameikanusha Haki ilipo wajia. Basi zitawajia khabari za yale waliyo
kuwa wakiyakejeli.
6. Jee, hawaoni vizazi vingapi tulivyo viangamiza kabla
7. Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangeli sema walio kufuru: Haya si chochote
ila ni uchawi dhaahiri.
8. Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na kama tungeli teremsha Malaika, basi bila ya shaka ingesha
hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula.
9. Na kama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka
tungeli mfanya kama binaadamu, na tungeli watilia matatizo yale wanayo
yatatiza wao.
10. Na hakika Mitume walio kabla yako walifanyiwa kejeli, lakini
walio wafanyia kejeli wakaja kuzungukwa na yale yale
waliyo kuwa wao wanayafanyia kejeli.
11. Sema: Tembeeni ulimwenguni, kisha mtazame ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
12. Sema: Ni vya nani viliomo katika mbingu na
katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye
amejilazimisha nafsi yake kurehemu. Hakika atakukusanyeni Siku ya Kiyama
isiyo kuwa na shaka. Walio jikhasiri
wenyewe hawaamini.
13. Na ni vyake vilio tulia usiku na
mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye
kujua.
14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye
ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha
wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza
wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa
washirikina.
15. Sema: Mimi naogopa adhabu ya Siku kubwa hiyo ikiwa nitamuasi
Mola wangu Mlezi.
16. Siku hiyo yule atakaye epushwa nayo adhabu hiyo atakuwa Mwenyezi
Mungu amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kulio wazi.
17. Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea hayo ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri,
basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila kitu.
18. Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, na
ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari zote.
19. Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi
Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na
nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi
na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii
hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni
mbali na mnao washirikisha.
20. Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua haya
21. Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi
Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika
madhaalimu hawafanikiwi.
22. Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio
shirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai?
23. Kisha hautakuwa udhuru wao ila ni
kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina.
24. Tazama jinsi wanavyo jisemea uwongo wenyewe. Na
yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua.
25. Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na
tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si
chochote ila hadithi za watu wa kale.
26. Nao huwazuia watu, na wao wenyewe
wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu,
wala wao hawatambui.
27. Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema:
Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini.
28.
29. Na walisema: Hakuna mengine ila maisha
yetu haya ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa.
30. Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi,
akawaambia: Je, si kweli haya? Na wao
watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu ni kweli.
Yeye atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile
mlivyo kuwa mnakataa.
31. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu,
mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa
tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo
32. Na maisha ya dunia si chochte ila ni
mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni
bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini?
33. Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao
hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi
Mungu.
34. Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla
yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa,
mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa
kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka
zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao.
35. Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao,
basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi
kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli
wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua.
36. Hakika wanao kubali ni wale wanao
sikia. Na ama wafu Mwenyezi Mungu atawafufua, na kisha
kwake Yeye ndio watarejeshwa.
37. Na wamesema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini
wengi wao hawajui.
38. Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma
39. Na walio kanusha Ishara zetu ni viziwi
na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye, na humweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye.
40. Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni
hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni
wakweli?
41. Bali Yeye ndiye mtakaye mwomba, naye atakuondoleeni mnacho
mwombea akipenda. Na mtasahau hao mnao wafanya washirika
wake.
42. Na kwa yakini tulipeleka Mitume kwa kaumu
zilizo kuwa kabla yako, kisha tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate
kunyenyekea.
43. Kwa nini wasinyenyekee ilipo wafika adhabu yetu? Lakini nyoyo
zao zilikuwa ngumu, na Shet'ani akawapambia waliyo
kuwa wakiyafanya.
44. Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila
kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuliwashika kwa
ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa.
45. Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
46. Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona
kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiye
kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza
Ishara, kisha wao wanapuuza.
47. Sema: Mwaonaje, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhaahiri, jee wataangamizwa isipo kuwa
walio dhulumu?
48. Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni
wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema
haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
49. Na walio kanusha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa
walivyo kuwa wakipotoka.
50. Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila
yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na
mwenye kuona. Basi hamfikiri?
51. Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa
Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili
wapate kuchamngu.
52. Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo,
hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.
53. Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa
wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao shukuru?
54. Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu
alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba
atakaye fanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha
akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye maghfira na
Mwenye kurehemu.
55. Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili
ibainike njia ya wakosefu.
56. Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya
Mwenyezi Mungu. Sema: mimi sifuati matamanio yenu.
Hivyo nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa
walio ongoka.
57. Sema: Mimi nipo kwenye sharia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi
sinacho hicho mnacho kihimiza. Hapana hukumu ila
ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni
Mbora wa kuhukumu kuliko wote.
58. Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha
katwa shauri baina yangu na nyinyi. Na
Mwenyezi Mungu anawashinda wote kuwajua madhaalimu.
59. Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila
analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala
kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha.
60. Naye ndiye anaye kufisheni usiku, na
anakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo
yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya.
61. Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na
hukupelekeeni waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu
humfisha, nao hawafanyi taksiri.
62. Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake.
Naye ni Mwepesi kuliko wote wanao hisabu.
63. Sema: Ni nani anaye kuokoeni katika
64. Sema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka hayo, na kutoka kila
mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha!
65. Sema: Yeye ndiye Muweza wa kukuleteeni
adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au kukuleteeni fujo la
mfarakano, na kuwaonjesha baadhi yenu jeuri ya wenzao. Tazama vipi tunavyo
zieleza Aya ili wapate kufahamu.
66. Na watu wako wameikanusha, nayo ni
Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu.
67. Kila khabari ina kipindi chake. Nanyi mtakuja jua.
68. Na unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka
waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani
akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu
madhaalimu.
69. Wala wamchao Mungu hawana jukumu lolote kwao, lakini ni
kukumbusha, asaa wapate
kujiepusha.
70. Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije
nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo yachuma, nayo
haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa
kila fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa
sababu ya yale waliyo yachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
71. Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala
hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu
kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza
katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu,
wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa
Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa
Mola Mlezi wa viumbe vyote,
72. Na mshike Sala, na mcheni Yeye, na
kwake Yeye ndiko mtako kusanywa.
73. Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi
kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake
Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye
ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari.
74. Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya
masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi
nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi.
75. Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa
mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
76. Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipo tua akasema: Siwapendi wanao
tua.
77. Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi
wangu. Ulipotua akasema:
78. Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi
wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema:
Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia
ushirikina.
79. Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba
mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa
washirikina.
80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi
Mungu, na hali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao
washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu.
Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi
je, hamkumbuki?
81. Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi
hamkhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na
kitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi kundi gani katika mawili haya
lina haki zaidi kupata amani,
82. Wale ambao wameamini, na
hawakuchanganya imani
83. Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo
tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na
Mwenye ujuzi.
84. Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na
Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na
Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema.
85. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema.
86. Na Ismail, na Al Yasaa, na Yunus, na
Lut'. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu wote.
87. Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao
na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa kwenye
Njia iliyo nyooka.
88. Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa
wakiyatenda.
89. Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na
Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa.
90. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya
91. Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa
haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu
chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa
mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa
hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache
wacheze katika porojo lao.
92. Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha,
kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa
Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao
wanazihifadhi Sala zao.
93. Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi
Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali
hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama
alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona madhaalimu wanavyo kuwa
katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea
mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu
yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
94. Nanyi mlitujia wapweke
95. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo
ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa?
96. Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa
mapumziko na utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa
hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi.
97. Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyota ili
mwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi
kwa watu wanao jua.
98. Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na
nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia.
Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao
fahamu.
99. Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje
zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada
yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga,
yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini.
100. Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya
ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike.
Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo
mbandikiza nayo!
101. Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi
bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na
mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.
102. Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu
ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila
kitu.
103. Macho hayamfikilii bali Yeye
anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye
khabari.
104. Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa
Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake
mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si
mtunzaji wenu.
105. Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao
wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao
jua.
106. Fuata uliyo funuliwa kutoka kwa Mola
wako Mlezi. Hapana mungu ila Yeye. Na jitenge na washirikina.
107. Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si
mlinzi juu
108. Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu,
wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri
bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo
vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao
Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.
109. Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa
viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa
zitapo kuja hawato amini.
110. Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho
111. NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na
maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado
wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao
wamo ujingani.
112. Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya
kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako
Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na
wanayo yazua.
113. Na ili nyoyo za wasio amini Akhera
zielekee hayo, nao wayaridhie na wayachume wanayo yachuma.
114. Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye
kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua
ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki.
Basi usiwe katika wanao tia shaka.
115. Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa
kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake.
Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
116. Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila
dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.
117. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua walio
potea Njia yake, na ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua
walio hidika.
118. Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa
mnaziamini Aya zake.
119. Na kwa nini msile katika walio somewa
jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni,
isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio
120. Na acheni dhambi zilizo dhaahiri na
zilizo fichikana. Hakika wanao chuma dhambi watalipwa kwa
waliyo kuwa wakiyachuma.
121. Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu.
Kwani huo ni upotofu. Na kwa
yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na
mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina.
122. Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru
inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni
123. Kadhaalika katika kila mji tumewajaalia wakubwa wa wakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala
hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao hawatambui.
124. Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe
mfano wa walio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi
Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao
walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi
Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.
125. Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia
kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee
hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana,
126. Na hii ndiyo Njia ya Mola wako Mlezi Iliyo nyooka.
Tumezipambanua Aya kwa watu wanao kumbuka.
127. Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola
Mlezi wao. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya
waliyo kuwa wakiyatenda.
128. Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya
majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika
wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu!
Tulinufaishana sisi na wao. Na
tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto
ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo
Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye
hikima, na Mwenye kujua.
129. Ndio kama hivi tunawaelekeza madhaalimu
wapendane wao kwa wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyachuma.
130. Enyi makundi ya majini na watu! Je,
hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe
wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao
watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya
maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba
walikuwa makafiri.
131. Hayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa wa kuiangamiza
miji kwa dhulma, hali wenyewe
wameghafilika.
132. Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na
yale waliyo yatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.
133. Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda
atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu,
134. Bila ya shaka hayo mnayo ahidiwa yatafika tu, wala nyinyi hamtaweza
kuyaepuka.
135. Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na
hakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na
makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa.
136. Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimea na wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi
Mungu - kwa madai
137. Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika
washirikina kuwauwa watoto wao ili kuwaangamiza na
kuwavurugia dini
138. Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii
ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai
139. Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni
kwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharimishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Mwenyezi Mungu
atawalipa kwa maelezo
140. Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa
upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo
waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala
hawakuwa wenye kuongoka.
141. Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja,
na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda
mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni
matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya
kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye
hawapendi watumiayo kwa fujo.
142. Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi
Mungu, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni
adui yenu dhaahiri.
143. Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume
wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni
kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.
144. Na wawili katika ngamia, na wawili
katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au
waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo
Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni
nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili
ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu
hawahidi watu madhaalimu.
145. Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa
mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au
damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu
kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola
wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
146. Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila
mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi
tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo
yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa
sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.
147. Wakikukanusha basi wewe sema: Mola Mlezi wenu ni
Mwenye rehema iliyo enea. Wala haizuiliki adhabu yake kwa
watu wakhalifu.
148. Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka
tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote.
Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla
149. Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na
150. Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu
ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala
usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine.
151. Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi.
Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu
ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo
amekuusieni ili myatie akilini.
152. Wala msiyakaribie mali ya yatima ila kwa njia ya wema kabisa, mpaka afikilie utu-uzima. Na timizeni vipimo na
mizani kwa uadilifu. Sisi hatumkalifishi mtu ila kwa
kadiri ya uwezo wake. Na msemapo semeni kwa uadilifu
ingawa ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu itekelezeni.
Hayo amekuusieni ili mpate kukumbuka.
153. Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu
Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili
mpate kuchamngu.
154. Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia
(neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na
rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi.
155. Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha,
kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili
mrehemewe.
156. Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa
Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa
wakiyasoma.
157. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa
waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa
Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa
zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na
akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara
zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
158. Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako
Mlezi, au zifike baadhi ya
Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako
Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au
amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.
159. Hakika walio igawa Dini yao na wakawa makundi makundi, huna ukhusiano nao wowote. Bila ya shaka shauri
160. Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na
afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao
hawatadhulumiwa.
161. Sema: Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi
ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila
ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa
kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa
viumbe vyote.
163. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.
164. Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi
haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba
mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa
mkikhitalifiana.
165. Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua
baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili
akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni
Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu