72 - AL - JINN
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini
lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala
hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana
mke wala mwana.
4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo
ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi
Mungu.
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta
kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa
Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu
na vimondo.
9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili
kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
10. Nasi hatujui
11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni
kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
12. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala
hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
13. Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini
Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.
14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao
acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.
15. Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.
16. Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli
wanywesha maji kwa wingi,
17.
18. Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote
pamoja na Mwenyezi Mungu.
19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao
walikuwa karibu kumzonga!
20. Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi
Yeye na yeyote.
21. Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
22. Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu,
wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.
23. Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake.
Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa
Jahannamu wadumu humo milele.
24. Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani
mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.
25. Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu
Mlezi atayawekea muda mrefu.
26. Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri
yake,
27. Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi
mbele yake na nyuma yake.
28. Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi,
na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.