77 - AL - MURSALAAT
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
2. Na zinazo vuma kwa kasi!
3. Na zikaeneza maeneo yote!
4. Na zinazo farikisha zikatawanya!
5. Na zinazo peleka mawaidha!
6. Kwa kuudhuru au kuonya,
7. Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
8. Wakati nyota zitakapo futwa,
9. Na mbingu zitakapo pasuliwa,
10. Na milima itakapo peperushwa,
11. Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
12. Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
13. Kwa siku ya kupambanua!
14. Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
15. Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
16. Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
17. Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
18. Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
19. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
20. Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
21. Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
22. Mpaka muda maalumu?
23. Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
24. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
25. Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
26. Walio hai na maiti?
27. Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na
tunakunywesheni maji matamu?
28. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
29. Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
30. Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
31. Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
32. Hakika Moto huo unatoa macheche
33.
34. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
35. Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
36. Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
37. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
38. Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio
tangulia.
39. Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
40. Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
41. Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
42. Na matunda wanayo yapenda,
43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa
mkiyatenda.
44. Hakika ndio
45. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
46. Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni
wakosefu!
47. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
48. Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
49. Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
50. Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?