8 - AL - ANFAAL
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni
ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na
suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa
nyinyi ni Waumini.
2. Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo
zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
3. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa
katika yale tunayo waruzuku.
4. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na
maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.
5. Kama Mola wako Mlezi alivyo kutoa nyumbani kwako kwa Haki, na hakika kundi moja la Waumini linachukia.
6. Wanajadiliana nawe kwa jambo la Haki baada ya kwisha bainika,
7. Na Mwenyezi Mungu alipo kuahidini kuwa moja katika makundi
mawili ni lenu. Nanyi mkapenda lisilo na nguvu ndio liwe lenu; na Mwenyezi Mungu
anapenda ahakikishe Haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri.
8.
9. Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni
kuwa: Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu wanao fuatana
mfululizo.
10. Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili
nyoyo zenu zituwe. Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.
11. Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na
akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni
uchafu wa Shet'ani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu
yenu.
12. Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja
nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio
kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za
vidole.
13. Hayo ni kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na
mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi Mwenyezi Mungu ni Mkali wa
kuadhibu.
14. Ndio hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu
ya Moto.
15. Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie
mgongo.
16. Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu
za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi
Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.
17. Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na
wewe hukutupa, walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye tupa, ili awajaribu Waumini
majaribio mema yatokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Msikizi na
Mjuzi.
18. Ndio hivyo! Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha
vitimbi vya makafiri.
19.
20. Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe
naye, nanyi mnasikia.
21. Wala msiwe kama wale wanao sema: Tumesikia, na kumbe
hawasikii.
22. Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni vile viziwi na
bubu visio tumia akili zao.
23. Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao ange
wasikilizisha, na lau ange wasikilizisha wangeli geuka wakapuuza.
24. Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo
kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu
huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu
mtakusanywa.
25. Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke
26. Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, mkionekana wanyonge katika
nchi, mnaogopa watu wasikunyakueni, naye akakupeni pahala pazuri pa kukaa, na
akakutieni nguvu kwa nusura yake, na akakupeni riziki nzuri ili mpate
kushukuru.
27. Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala
msikhini amana zenu, nanyi mnajua.
28. Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na
kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.
29. Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na
atakufutieni makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila
kubwa.
30. Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au
wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi
Mungu ndiye mbora wa mipango.
31. Na wanapo somewa Aya zetu, wao husema: Tumesikia. Na lau tungeli
penda tunge sema kama haya. Haya si chochote ila hadithi za watu wa kale
tu.
32. Na walipo sema: Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo
kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo
chungu.
33. Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu nawe umo pamoja nao, wala
Mwenyezi Mungu si wa kuwaadhibu na hali ya kuwa wanaomba msamaha.
34. Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali
ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa ndio walinzi
wake, bali walinzi wake hawakuwa ila wacha-Mngu tu. Lakini wengi katika wao
hawajui.
35. Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga
miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
36. Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya
Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha
watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.
37. Ili Mwenyezi Mungu apate kuwa pambanua walio waovu na walio
wema, na kuwaweka waovu juu ya waovu wengine, na kuwarundika wote pamoja, na
kuwatupa katika Jahannam. Hao ndio walio khasirika.
38. Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha
pita. Na wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani.
39. Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu
anayaona wanayo yatenda.
40. Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola
wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema.
41. NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja
katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na
masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo
yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili.
Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
42. Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya
bonde, na wao wakawa ng'ambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na
ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili
Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie
wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili
zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
43. Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache
- na lau angeli kuonyesha kuwa ni wengi, mngeli ingiwa na woga, na mngeli
zozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu kakuvueni. Hakika Yeye ni
Mwenye kuyajua yalio vifuani.
44. Na mlipo kutana akakuonyesheni machoni mwenu kuwa wao ni
wachache, na akakufanyeni nyinyi ni wachache machoni mwao, ili Mwenyezi Mungu
atimize jambo lilio kuwa liwe. Na mambo yote hurejezwa kwa Mwenyezi Mungu.
45. Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na
mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa.
46. Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane
mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu
pamoja na wanao subiri.
47. Wala msiwe kama wale walio toka majumbani mwao kwa fakhari na
kujionyesha kwa watu, na wakawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi
Mungu ameyazunguka yote wanayo yafanya.
48. Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia:
Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana
majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona
msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa
kuadhibu.
49. Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao:
Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi
hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima.
50. Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga
nyuso zao na migongo yao, na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto!
51. Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono
yenu, na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.
52. Kama ada ya watu wa Firauni na walio kuwa kabla yao -
walizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa sababu
ya madhambi yao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na mkali wa
kuadhibu.
53. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo
waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika
Mwwnyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
54. Ni kama ada ya watu wa Firauni na walio kabla yao -
walizikanusha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawateketeza kwa madhambi yao.
Na tukawazamisha watu wa Firauni. Na wote walikuwa wenye kudhulumu.
55. Hakika vinyama vilio viovu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni
wale wanao kufuru, basi hao hawaamini;
56. Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja
ahadi yao kila mara, wala hawamchi Mungu.
57. Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma
58. Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi
59. Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele.
La, wao hawatashinda.
60. Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio
fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu,
na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote
katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.
61. Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu.
Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
62. Na wakitaka kukukhadaa basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Kwani
Yeye ndiye aliye kuunga mkono kwa nusura yake na kwa Waumini.
63. Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo
duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye
waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
64. Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na Waumini walio
kufuata.
65. Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu
ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia
watawashinda elfu moja katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio
fahamu.
66. Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu
kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri
watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa
idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
67. Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda
baraabara katika nchi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka
Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima.
68. Lau isingeli kuwa hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa
Mwenyezi Mungu ingeli kupateni adhabu kubwa kwa vile mlivyo chukua.
69. Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye
kurehemu.
70. Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi
akiona kheri yoyote nyoyoni mwenu atakupeni bora kuliko vilivyo chukuliwa
kwenu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
71. Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana
Mwenyezi Mungu kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu
ni Mwenye kujua Mwenye hikima.
72. Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya
Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, na wale walio toa mahala pa kukaa, na
wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walio amini lakini
hawakuhama, nyinyi hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame.
Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo
kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu
anayaona mnayo yatenda.
73. Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo
fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa.
74. Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya
Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa
kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.
75. Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi
pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana
wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.