85 - AL - BURUUJ
KWA JINA
LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Naapa kwa mbingu yenye Buruji!
2. Na kwa siku iliyo ahidiwa!
3. Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
4. Wameangamizwa watu wa makhandaki
5. Yenye moto wenye kuni nyingi,
6. Walipo kuwa wamekaa hapo,
7. Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia
Waumini.
8. Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi
Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa,
9. Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni
shaahidi wa kila kitu.
10. Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha
hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya
kuungua.
11. Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye
12. Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
13. Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
14. Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
15. Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu,
16. Atendaye ayatakayo.
17. Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi?
18. Ya Firauni na Thamudi?
19. Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
20. Na Mwenyezi Mungu nyuma
21.
22. Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.