92 - AL - LAYL
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Naapa kwa usiku unapo funika!
2. Na mchana unapo dhihiri!
3. Na kwa Aliye umba dume na jike!
4. Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni
mbali mbali.
5. Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
6. Na akaliwafiki lilio jema,
7. Tutamsahilishia yawe mepesi.
8. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na
haja ya wenzake,
9. Na akakanusha lilio jema,
10. Tutamsahilishia yawe mazito!
11. Na
12. Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
13. Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
14. Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
15. Hatauingia ila mwovu kabisa!
16. Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
17. Na mchamngu ataepushwa nao,
18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
20. Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
21. Naye atakuja ridhika!