98 - AL - BAYYINAH
KWA
JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
1. Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina
waache walio nayo mpaka iwajie bayana,
2. Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa
zilizo takasika,
3. Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka.
4. Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila
baada ya kuwajia hiyo bayana.
5. Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa
kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na
watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
6. Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa
Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
7. Hakika walio amini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.
8. Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo