Home / Quran Translations / Kiswahili / Compare / Nuh
Text size
A−
100%
A+
Reset
◐
Change language
Choose a language…
English — English
Qafar af — Afar
Asante / Akan — Akan (Asante)
Shqip — Albanian
ⵜⴰⵎⴰⵣⵉⵖⵜ — Amazigh
አማርኛ — Amharic
অসমীয়া — Assamese
Azərbaycanca — Azerbaijani
বাংলা — Bangla
Tamaziɣt — Berber / Tamazight
Bosanski — Bosnian
براہوی — Brahui
Български — Bulgarian
မြန်မာ — Burmese
Нохчийн — Chechen
Chichewa — Chichewa
中文 — Chinese
Адыгэбзэ — Circassian / Kabardian
Čeština — Czech
Dansk — Danish
ދިވެހި — Dhivehi
Nederlands — Dutch
Suomi — Finnish
Français — French
Fulfulde — Fulani
ქართული — Georgian
Deutsch — German
Ελληνικά — Greek
ગુજરાતી — Gujarati (legacy Ghajariya)
Hausa — Hausa
हिन्दी — Hindi
Bahasa Indonesia — Indonesian
Iranon — Iranon (legacy)
Italiano — Italian
日本語 — Japanese
ಕನ್ನಡ — Kannada
کٲشُر — Kashmiri
Қазақша — Kazakh
ខ្មែរ — Khmer
한국어 — Korean
Kurdî — Kurdish
Кыргызча — Kyrgyz
Lingala — Lingala
Luganda — Luganda
Македонски — Macedonian
Melayu — Malay
മലയാളം — Malayalam
Manipuri — Manipuri
Maranao — Maranao
Español (México) — Mexican Spanish
नेपाली — Nepali
Norsk — Norwegian
ߒߞߏ — N’Ko
Oromoo — Oromo
پښتو — Pashto
فارسی — Persian
Polski — Polish
Português — Portuguese
ਪੰਜਾਬੀ — Punjabi
Română — Romanian
Русский — Russian
ChiShona — Shona
سنڌي — Sindhi
සිංහල — Sinhala
Soomaali — Somali
Español — Spanish
Kiswahili — Swahili
Svenska — Swedish
Tagalog — Tagalog
Тоҷикӣ — Tajik
தமிழ் — Tamil
Татарча — Tatar
తెలుగు — Telugu
ไทย — Thai
ትግርኛ — Tigrinya
Türkçe — Turkish
اردو — Urdu
ئۇيغۇرچە — Uyghur
Oʻzbek — Uzbek
Tiếng Việt — Vietnamese
Yao — Yao
Yorùbá — Yoruba
isiZulu — Zulu
Translation comparison Compare Nuh Quran translations Compare up to three verified translation editions verse by verse, including editions in two different languages.
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ إِنَّآ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦٓ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌۭ ﴿1﴾
Al-Barwani Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.
قَالَ يَٰقَوْمِ إِنِّى لَكُمْ نَذِيرٌۭ مُّبِينٌ ﴿2﴾
Al-Barwani Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu,
أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ ﴿3﴾
Al-Barwani Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.
يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍۢ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿4﴾
Al-Barwani Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!
قَالَ رَبِّ إِنِّى دَعَوْتُ قَوْمِى لَيْلًۭا وَنَهَارًۭا ﴿5﴾
Al-Barwani Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana,
فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَآءِىٓ إِلَّا فِرَارًۭا ﴿6﴾
Al-Barwani Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.
وَإِنِّى كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوٓا۟ أَصَٰبِعَهُمْ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَٱسْتَغْشَوْا۟ ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا۟ وَٱسْتَكْبَرُوا۟ ٱسْتِكْبَارًۭا ﴿7﴾
Al-Barwani Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!
ثُمَّ إِنِّى دَعَوْتُهُمْ جِهَارًۭا ﴿8﴾
Al-Barwani Tena niliwaita kwa uwazi,
ثُمَّ إِنِّىٓ أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًۭا ﴿9﴾
Al-Barwani Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
فَقُلْتُ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارًۭا ﴿10﴾
Al-Barwani Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
يُرْسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًۭا ﴿11﴾
Al-Barwani Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَٰلٍۢ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّٰتٍۢ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَٰرًۭا ﴿12﴾
Al-Barwani Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًۭا ﴿13﴾
Al-Barwani Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?
وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا ﴿14﴾
Al-Barwani Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?
أَلَمْ تَرَوْا۟ كَيْفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبْعَ سَمَٰوَٰتٍۢ طِبَاقًۭا ﴿15﴾
Al-Barwani Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
وَجَعَلَ ٱلْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًۭا وَجَعَلَ ٱلشَّمْسَ سِرَاجًۭا ﴿16﴾
Al-Barwani Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?
وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ نَبَاتًۭا ﴿17﴾
Al-Barwani Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.
ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًۭا ﴿18﴾
Al-Barwani Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ بِسَاطًۭا ﴿19﴾
Al-Barwani Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.
لِّتَسْلُكُوا۟ مِنْهَا سُبُلًۭا فِجَاجًۭا ﴿20﴾
Al-Barwani Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.
قَالَ نُوحٌۭ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِى وَٱتَّبَعُوا۟ مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارًۭا ﴿21﴾
Al-Barwani Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.
وَمَكَرُوا۟ مَكْرًۭا كُبَّارًۭا ﴿22﴾
Al-Barwani Na wakapanga vitimbi vikubwa.
وَقَالُوا۟ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّۭا وَلَا سُوَاعًۭا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًۭا ﴿23﴾
Al-Barwani Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.
وَقَدْ أَضَلُّوا۟ كَثِيرًۭا ۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلًۭا ﴿24﴾
Al-Barwani Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
مِّمَّا خَطِيٓـَٰٔتِهِمْ أُغْرِقُوا۟ فَأُدْخِلُوا۟ نَارًۭا فَلَمْ يَجِدُوا۟ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارًۭا ﴿25﴾
Al-Barwani Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.
وَقَالَ نُوحٌۭ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى ٱلْأَرْضِ مِنَ ٱلْكَٰفِرِينَ دَيَّارًا ﴿26﴾
Al-Barwani Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا۟ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓا۟ إِلَّا فَاجِرًۭا كَفَّارًۭا ﴿27﴾
Al-Barwani Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
رَّبِّ ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِىَ مُؤْمِنًۭا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارًۢا ﴿28﴾
Al-Barwani Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.