Skip to content
Text size 100%
Kiswahili · Surah 85

Al-Buruj — Swahili Translation

The Mansions of the Stars · 22 verses · Swahili Translation - Rowad Translation Center.

Al-Buruj · Swahili Translation - Rowad Translation CenterVerse 1 of 22
Jump to verse
Search translation

Search the locally cached translation.

Verses of Al-Buruj

1

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْبُرُوجِ

Ninaapa kwa mbingu yenye nyota kubwa kubwa!

2

وَٱلْيَوْمِ ٱلْمَوْعُودِ

Na kwa Siku iliyoahidiwa!

3

وَشَاهِدٍۢ وَمَشْهُودٍۢ

Na kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!

4

قُتِلَ أَصْحَٰبُ ٱلْأُخْدُودِ

Wameangamizwa watu wa makhandaki.

5

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلْوَقُودِ

Yenye moto wenye kuni nyingi.

6

إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌۭ

Walipokuwa wamekaa hapo.

7

وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌۭ

Na wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini.

8

وَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ

Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.

9

ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍۢ شَهِيدٌ

Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.

10

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُوا۟ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا۟ فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ ٱلْحَرِيقِ

Hakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.

11

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمْ جَنَّٰتٌۭ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْكَبِيرُ

Hakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani za mbinguni zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

12

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.

13

إِنَّهُۥ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ

Yeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejesha tena.

14

وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلْوَدُودُ

Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi.

15

ذُو ٱلْعَرْشِ ٱلْمَجِيدُ

Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu.

16

فَعَّالٌۭ لِّمَا يُرِيدُ

Atendaye ayatakayo.

17

هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْجُنُودِ

Je! Zimekufikia habari za Majeshi?

18

فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ

Ya Firauni na Thamudi?

19

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى تَكْذِيبٍۢ

Lakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha.

20

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطٌۢ

Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.

21

بَلْ هُوَ قُرْءَانٌۭ مَّجِيدٌۭ

Bali hii ni Qur-ani tukufu.

22

فِى لَوْحٍۢ مَّحْفُوظٍۭ

Katika Ubao uliohifadhiwa.

Al-Buruj in other Swahili translations

Source: QuranEnc.com · Version 1.0.5. Translation text is shown without rewriting.
Quran recitationReady
Open audio